Mada zetu

kibamia

kibamia.png

Tatizo hili limedhalilisha wanaume wengi. Na imepelekea hata wengine kuvunja mahusiano/ndoa zao. Kwa upande mwingine tatizo hili limepelekea baadhi ya wanaume kuogopa hata kujihusisha na mapenzi na wanawake wanaowafahamu kwa sababu ya kuogopa aibu na kudhalilishwa. Aibu hutokea pale ambapo mwanamke asiye na staha kumwanika kwa kutoa siri yake.

Sio kitu rahisi. Mtu anaweza hata kushindwa kufanya kazi zake kwa sababu hii. Kwa sababu anakuwa na aibu ambayo anahisi kama dunia nzima inamwangalia uchi wake. Utasikia maneno, mwanaume utakuwa wewe!. Na hii inawafanya wengi kuishia kwa wanawake wanaojiuza ili kukidhi haja zao kwa sababu ni ngumu kuwa na mahusiano na wanawake wanaowafahamu wasije wakawaanika labda siku wakiachana au kama ikitokea kukosana.

Uume wenye ukubwa gani ndio kibamia?

Kulingana na utafiti ulifanywa na British Journal of Urology international, wastani wa ukubwa wa uume ni nchi 5.1 (sentimita 12.9). Na mtu mwenye uume chini ya nchi 3 (sentimeta 7.5) ndio ambao ni uume mdogo yaani kibamia. Vipimo hivi vifanyike uume ukiwa umesimama, pima kuanzia juu kabisa mwisho wa kichwa cha uume mpaka kwenye shina.

Mara mwingi wanaume wamekuwa wakiona maumbile yao kuwa mdogo kuliko uhalisia wake. British Journal of Urology international, katika utafiti wao wanasema kuwa 45% ya wanaume wanaamini kuwa uume wao ni mdogo lakini tafiti zinaonesha wanaume wenye tatizo hili ni wachache sana (0.6%).

Kwa upande wa wanawake 85% walisema wanaridhishwa na ukubwa wa mmaumbile ya wenzi wao. Lakini nusu ya wanaume (45%) walikuwa na mashaka na ukubwa wa maumbile yao. Tatizo la uume mdogo (kibamia) sio kubwa kama linavyofikiriwa na watu. Tatizo lipo kwenye saikolojia zaidi kuliko kimwili.

Sababu za uume kuwa mdogo sana (kibamia)

  1. Magonjwa ya utotoni

Hii ni sababu ya muhimu zaidi katika mfululizo wa sababu zenye mashiko ya uume kuwa mdogo. Kukua kwa uume huanza mapema sana mtoto anapozaliwa. Endapo kutatokea tatizo wakati huu wa ukuaji mtu anaweza kuwa na uume mdogo hata ukubwani kama tatizo hilo halitashughulikiwa. Baadhi ya matatizo yanayoweza kujitokeza wakati wa ukuaji ni pamoja na magonjwa ya tezi za pituitari na haipothalamasi. Matatizo ya uzalishaji wa (kemikali za mwili) homoni  kama testosterone.

  1. Kupiga punyeto kwa muda mrefu

Kufanya punyeto kwa muda mrefu pia hudhoofisha misuli ya uume na kuifanya kuwa mwembamba na kurudi ndani.

  1. Kuugua chango la uzazi/kiume
  2. Kurithi

Mtu anapozaliwa anapata vinasaba ambavyo ndivyo vinaamua mtu kuonekana kama alivyo. Kwa hiyo hata namna uume utakavyoumbika ni kwa sababu ya vile vinasaba ambavyo unaweza ukawa umerithi kutoka kwa wazazi/ndugu zako.

  1. Kitambi

Mafuta yanapojaa tumboni pia inaweza kuwa ni sababu ya kufanya sehemu ya uume kufunikwa na hivyo kuonekana mdogo. Sio kwa wote inatokea hivyo lakini ni sababu mojawapo.

  1. Mtazamo

Ukiangalia maumbile yako kwa kuyatazama kutoka juu mara nyingi yanaonekana madogo kuliko yalivyo hasa. Na hii hudhirika pale ambapo utawaangalia wengine. Ili kujua mwonekano halisi  wa uume wako unaweza kusimama mbele ya kioo na kujiangalia. Utaona kwamba  ukubwa wake sio mdogo kama ambavyo ulifikiri.

Changamoto nyingine hapa ni tabia ya kuangalia picha za ngono. Mtu anayeangalia picha za ngono anapojaribu kulinganisha ukubwa wa maumbile yao na yake, duuh! Anakuwa na wasiwasi sana kama ataweza kumridhisha mwenzi wake. Lakini mawazo haya ni potofu na wala usijikute katika dimbwi la kutafuta dawa ya kuongeza maumbile kwani dawa hizo zinaweza kukuletea madhara baadaye.

Jikubali, jiamini na mwelimishe mwenzi wako kuhusu haya ili asiwe na dhana potofu ya mtaani kuhusu kibamia. Nakutakia kila la kheri katika mahusiano yako!

Leave a Comment

Your email address will not be published.