Mada zetu

hatari

Usile usiku sana ni hatariKwa kawaida asubuhi kabla ya kwenda kufanya kazi unatakiwa kupata chakula kingi cha kushiba kabisa. Itakusaidia kutokuwa na hamu ya kula kula katikati ya milo (maana vyakula vingi vilivyopo katikati ya milo huwa ni vile vyenye sukari nyingi sana na mafuta kwa wingi — HATARI).
Kama unapenda na unapanga kweli kutokulakula katikati ya milo utapata tabu sana kufanya maamuzi ya kujizuia pale unapokutana na chakula lakini njia salama kula vizuri kabisa asubuhi na hutokuwa na hamu ya kula kula.


Sababu nyingine kwa nini ule vizuri asubuhi, chakula kilicholiwa asubuhi hutumiwa na mwili wakati wa shughuli za siku. Lakini mchana kiwango cha chakula kipunguwe kidogo ukilinganisha na kile ulichokula asubuhi.

Jifunze Katika Utafiti Huu

Makundi 2 ya wanaume waliojitolea walipewa chakula kinachofanana na kulingana kwa wiki 2, lakini tofauti ni kwamba kundi A walikitumia kile chakula asubuhi na kundi B walikitumia usiku.
Kundi A walipungua uzito; kundi B waliongeza. Makundi yakabadlishwa, na matokeo yakawa Yale yale. Kwa nini? Kwa sababu chakula kinacholiwa usiku hutunzwa kama mafuta badala ya kutumika kwa ajili ya shughuli zingine kama ilivyokuwa kwa kile cha asubuhi.


Pia usiku unapolala vichocheo vinavyohusika na usingizi hupunguza sana au kuzuia kabisa shughuli za umeng’enyaji wa chakula usiendelee. Matokeo yake ni kwamba chakula kinachacha tumboni na kulundikana na hivyo shida kama tumbo kujaa gesi, tumbo kuwa kubwa sana, na magonjwa mengine kama saratani yanaweza kuibuka.


Kama ukisahau yote hayo kumbuka hili, kula chakula kingi na bora zaidi asubuhi, cha kawaida mchana na kidogo sana usiku


Kwa wale walio na mchakato wa kupunguza uzito ni vema usiku wasile itawasaidia au kama itawalazimu kula, ni vema wakatumia supu, juisi ya matunda au kula matunda pekee yake.

dr nature anakuletea (1)

The old adage | “Breakfast like a king, lunch like a prince, sup like a pauper”

Leave a Comment

Your email address will not be published.