Mada zetu

punguza uzito hatua kwa hatua


Uzito mkubwa au mdogo kupita kiasi ni hatari kiafya.
Kiwango cha uzito kuwa mdogo au mkubwa ninachokizungumzia hapa kinaweza kupimwa kwa namna 2 ili kuwa na uhakika.

Njia ya kwanza unaweza kupima kwa kutumia BMI (Body Mass Index) ambapo unachukua uzito wako (kg) unagawanya kwa kipeo cha pili cha urefu wako katika kipeo cha pili cha mita (m)².

Majibu yako utakayopata yalinganishe na haya

BMI MAONI
Chini ya 18.5 Uzito mdogo kupita kiasi
18.5-24.9 Kawaida
25-29.9 Uzito mkubwa kupita kiasi
30+ Kiriba tumbo


Aina hii ya upimaji ina changamoto kwa baadhi ya watu mfano wanaofanya mazoezi sana misuli inakuwa mikubwa sana na BMI zinaonekana kuwa juu lakini hawana kiriba tumbo. Kwa wazee na watu wembamba sana wanaweza kuonekana wanauzito mdogo kupita kiasi kama ukitumia BMI lakini si kweli.


Ili kuhakikisha kuna njia nyingine mtu anaweza kujipima kujua yupo upande gani.

Hapa tunatumia WHR (Waist to Hip Ratio). Unapima kwa kutumia futi kamba juu tumboni juu ya kidogo ya kitovu (sehemu nyembamba kuliko zote tumboni), na pia unapima kiunoni/hips (sehemu Nene kuliko zote kiunoni). Halafu gawanya ile ya tumboni na kiunoni. Kisha linganisha na hizi.


Wanawake ikizidi 0.8 ni hatari na kwa wanaume ikizidi 0.95 ni hatari.


Hii tunaifanya kwa sababu watu ambao wanamaumbo ya tofaa (apple) kwa maana ya kwamba mafuta mengi yamelundamana tumboni kuliko sehemu zingine wanahatari zaidi ya kupata magonjwa ya moyo, kisukari, kiharusi, saratani, matatizo ya mifupa n.k ukilinganisha na watu wenye maumbo ya pear kwa maana mafuta anayo mengi lakini yamesambaa karibu mwili wote.


UZITO MKUBWA NI HATARI SANA KWA SABABU UNAKUPELEKEA KUPATA MAGONJWA KAMA MOYO, KISUKARI, BAWASIRI, MIFUPA, SARATANI, SHINIKIZO LA JUU LA MOYO, INI, FIGO KADHALIKA UZITO MDOGO KUPITA KIASI SI SALAMA.


Kwa hiyo ukishajipima kwa njia hizo na kuhakikisha kuwa upo upande gani hapo sasa tunaweza kuanza safari ya kurejesha uzito katika usawa.
********************

Baada ya kujua nini maana ya uzito mkubwa na mdogo kupita kiasi na namna ya kupima, na kama ni mfuatiliaji mzuri naamini utakuwa umechukua hatua kujipima na sasa unafahamu upo upande gani.

Ikiwa haupo kwenye kiwango stahiki unapaswa kufuata haya ili kurudi katika hali ya uzito sahihi.

Kanuni Ya Msingi

Kila unapokula chakula kinatakiwa kutumika na mwili, kama ikitokea umekula chakula kingi na mwili ukatumia kidogo maana yake chakula kingine kinabadilishwa na kuhifadhiwa mwilini kama mafuta ambayo ndio yanayokufanya kuwa na uzito kupita kiasi.

Na kama chakula kinachofika kwenye damu ni kidogo kuliko mahitaji ya mwili, mwili utadhoofu na uzito mdogo kupita kiasi utaonekana.

Kwa hiyo, ili kuwa na uzito sahihi kanuni hii lazima izingatiwe.


Chakula kinachoingia =Chakula kinachotumika


UONGO KUHUSU KUPUNGUZA UZITO

Watu wengi hudanganyika eti kufanya mazoezi na kupunguza kula kunasaidia mtu kupunguza uzito hii sio kweli, nitaeleza kwa nini..

Mazoezi ni muhimu sana kwa ajili ya kuhamasisha kazi za mwili (metabolism) kufanya kazi barabara.
MF. Kama umekula sana ukafanya mazoezi maana yake unahamasisha kile chakula pamoja na kutumika kitengeneza nguvu kwa ajili ya mazoezi pia kusaidia shughuli zingine za mwili kufanya kazi vema, ikiwemo kubadili hicho chakula kilichozidi kuwa mafuta na uzito kuongezeka.


Sikatai, ni kweli mazoezi ni muhimu sana kwa ajili ya kusaidia kupunguza uzito lakini ufanisi wake ni pungufu ya 20% katika mchakato mzima.

Wala huna haja ya kujinyima chakula ili kupunguza uzito…


Fanya haya machache wewe mwenyewe utanipatia majibu kwamba ulipata uzito ulikuwa unataka..

  • Tumia wanga isiyochakatwa/ kukobolewa katika asili yake mfano Mchele wa brown, viazi, ngano isiyokobolewa, nafaka zisizokobolewa, n.k hivi vina nyuzinyuzi nyingi kwa hiyo huujaza mfumo wa chakula bila kutoa calories/nguvu nyingi sana kuliko hitaji la mwili.
  • Kula matunda kama yalivyo (si katika hali ya juisi) pia yananyuzinyuzi na huleta matokeo kama hapo juu.
  • Ongeza mbogamboga mbichi au zilizopitishwa kwenye mvuke (isiyopikwa sana) kadhalika kuna nyuzi nyuzi kwa kazi ileile.
  • Usisahau vyakula jamii ya Karanga na mbegu zote itakusaidia sana kupata protin salama kwa afya yako na pia kuleta hali ya kutosheka na Chakula.


HABARI NJEMA!

UNAWEZA UKALA SANA LAKINI BADO UKAPATA UZITO UNAOTAKIWA…

Utakuwa na msawazo wa kiasi cha nguvu kinachoingia na kila kinachotumika

Ufupisho kuhusu Chakula, wanga asili isiokobolewa, protini ya mimea kidogo na mafuta ya mimea kidogo sana. Pia mishipa ya damu itakuwa safi.


Kwa ufupi, ili kupunguza uzito: fuata mtindo huo wa Chakula nilioelekeza na Fanya mazoezi mepesi kidogo kidogo kila siku.

Unataka nini zaidi?

Usipofuata taratibu hizi nilizoelekeza, baadaye itakugharimu pesa nyingi kusaidiwa kupunguza uzito. Anza leo na jionee tofauti.

UNGETAMANI KUONGOZWA HATUA KWA HATUA KUPUNGUZA UZITO?

Jiunge leo na tovuti yetu kwa kujisajili kwa barua pepe yako hapa chini, kuna kozi maalumu tunaiandaa kwa ajili yako. Itakufaa sana!

Nature Care Uhakika 100%

#Vinasaba hupakia risasi mtindo wa maisha hulipua | Genes load the gun lifestyle pulls the trigger.

 

Leave a Comment

Your email address will not be published.