Mada zetu

Kaswende ni ugonjwa wa zinaa unaotibika. Husabishwa na bakteria wanaoitwa Treponema pallidum Kama usipotibiwa, unaweza kusababisha athari kubwa kiafya na hata kifo. Kulingana na Shirika la Afya Duniani (WHO), kila mwaka makadirio ya watu milioni 357 wana magonjwa ya zinaa yatokanayo na kisonono, klamidia na trichimoniasisi duniani. Katika idadi hii kubwa karibia milioni 1 ni wajawazito wenye kaswende. Kaswende inaweza kurithishwa kwa mtoto aliyeko tumboni. Katika mwaka 2012, kaswende ilisababisha matatizo ya uzazi 350,0000 na kuzaa mtoto aliyekufa.[1][2]

Mtu anapata maambukizi pale bakteria wanapofanikiwa kuvunja utando wa uteute kwenye uke, mdomo, pua na mkundu. Pia wanaweza kuingia kupitia kidonda au sehemu iliyochubuka.[3]

Kukutana kimwili na mtu aliyeathirika, japokuwa kwa njia nyingine tofauti na ngono inawezekana.  Ni muhimu kuugundua ugonjwa huu mapema na kuutibu kwa dawa sahihi. Njia sahihi ya kutibu kaswede ni kutumia dawa (antibaitiksi). Moja kati ya changamoto za ugonjwa wa kaswende ni kuwa unapelekea kuibuka kwa magonjwa mengine. Kaswende ni ugonjwa unaoweza kudumu katika kipindi cha maisha yote kama hautatibiwa na dawa yenye kuwaua hao bakteria.[4]

Kaswende haiwezi kuambukiza kwa kushiriki choo na mtu mwingine, kuvaliana nguo na mtu mwingine au kushiriki vyombo vya kulia na mtu mwingine.

Kumekuwa na ongezeko la maambukizi ya kaswende kwa mashoga katika miaka ya hiivi karibuni.[5][6]

Inaaminika kwamba kufikia mwaka wa 1999 watu milioni 12 walikuwa wameambukizwa kaswende ulimwenguni na zaidi ya asilimia 90 ya hali hizi kutoka kwa nchi zinazoendelea. Hali za kaswende zilipungua kwa kasi baada ya penisilini kupatikana kwa urahisi katika miaka ya 1940, lakini viwango vya maambukizi vimeongezeka tangu mwaka 2000 katika nchi nyingi. Mara nyingi kaswende hupatikana pamoja na virusi vinavyosababisha UKIMWI (VVU). Hii imehusishwa na sehemu ya matendo ya ngono yasiyokuwa salama kati ya wanaume wanaofanya ngono na wanaume wengine;Ongezeka la uasherati; ukahaba; na kupungua kwa matumizi ya kondomu[7]

Dalili za kaswende

Dalili za kaswende zinategemea hatua ya ugonjwa. Wagonjwa wengi wa kaswende wanafikiri kuwa hawana ugonjwa kwa sababu mwanzoni dalili hupotea zenyewe bila matibabu yoyote kabla hazijarudi kwa upya. Hata hivyo, bila matibabu yoyote bakteria wanaendelea kuushambulia mwili na kusababisha athari mbaya sana kiafya na hata kifo.

Hatua 4 za kaswende

 1. Hatua ya awali

Hatua hii huanza siku 10-90 baada ya kupata maambukizi ya bakteria wanaosababisha kaswende huku kwa wengi inatokea baada ya wiki 3. Dalili katika kipindi hiki ni;

 • Malengelenge madogo yanayotumbuka au vidonda vidogo; bila maumivu – hutokea eneo maambukizi yalipoanzia. Hii mara nyingi hutokea kwenye via vya uzazi, matako au mkundu, au kuzunguka mdomo. Hupotea/kupona vyenyewe kwa kutibiwa au bila matibabu kwa muda wa wiki 3-6. Muundo wa malengelenge haya unatofautiana mtu mmoja na mwingine. Kwa baadhi ya wanawake malengelenge yanaweza kutokea kwenye mlango wa kizazi na hivyo hayaonekani.
 • Kuvimba kwa matezi karibu na eneo lililoanza kupata maambukizi.

Kama kaswende haitatibiwa kwa dawa stahiki, dalili hizi zitapotea na ugonjwa utaingia katika haua ya pili.

 1. Hatua ya pili

Katika hatua hii, dalili zinakuwa mbaya zaidi. Ugonjwa unaenea kwenye ngozi, ini, tezi, misuli na ubongo. Wiki 6 hadi miezi 3 baada ya malengelenge kupona , vipele vitatookea kuonesha kuwa ni hatua ya 2 ya ugonjwa. Vipele hivi vinaweza kutokea kama vipele vikubwa visivyo na umbo maalumu (blotches)  au vilivyojongezwa (indented). Vinaweza kuwa na rangi ya pinki au kijivu iliyokolea. Vipele hivi kadhali hutofautiana mtu na mwingine.

Dalili katika hatua ya 2

 • Vipele kwenye viganja na malengeleenge kwenye wayo
 • Vipele kwenye mikono, miguu na mwili
 • Vialama vyeupe (kama viraka) mdomoni, ukeni na sehemu zingine zenye utando wa uteute.
 • Vialama vyenye rangi ya kijivu iliyokolea au pinki kwenye ngozi.
 • Vialama kama chunjuwa (warts) vinyevu kwenye via vya uzazi au kwenye mikunjo ya ngozi.
 • Homa
 • Kujisikia vibaya
 • Kukosa hamu ya kula
 • Kupungua uzito
 • Maumivu ya misuli
 • Maumivu ya maungio ya mifupa
 • Madonda ya koo
 • Nywele kunyonyoka
 • Kushindwa kuona vizuri
 • Kuchoka sana kupita kiasi

Kama ugonjwa huu hautatibiwa utaendelea katika hatua ya tatu.

 1. Hatua ya 3

Hatua hii ni inawachanganya wagonjwa wengi nawatafiti wengi. Katika kipindi hiki hakuna dalili yoyote inayoonekana lakini ugonjwa upo unaendelea mwilini.[8] Bakteria wanaendelea kuishi kwenye wengu na tezi. Ugonjwaa unaweza kukaa kwenye hatua hii kwa miaka mingi. Kulingana na tafiti, kama katika hatua hii ugonjwa hautatibiwa makadirio ya theluthi moja huendelea katika hatua ya mwisho ya ugonjwa.

 1. Hatua ya 4

Katika hatua hii kaswende inakuwa ugonjwa wa hatari sana. Hapa huathiri kwa kiwango kikubwa zaidi ubongo, moyo, mishipa ya damu, mfumo wa kati wa ufahamu, ini, mifupa na maungio ya mifupa. Hatua hii hutokea baada ya miaka 10-30 baada ya kupata maambukizi. Kuharibiwa kwa viungo, ubongo na mfumo wa kati wa fahamu vinaweza kupelekea mtu kufariki.[9]

Dalili katika hatua ya 4

Dalili zinatofautiana sana kutoka mtu mmoja na mwingine kutokana na kiungo gani kilichoathirika. Baadhi ya dalili zinazoonekana sana kwa wagonjwa wanaofika katika vituo vya afya ni pamoja na;

 • Kuharibika/kuumia kwa moyo
 • Magonjwa ya valvu
 • Uvimbe kwenye ini, ngozi na mifupa
 • Magonjwa ya mfumo wa kati wa neva za fahamu
 • Maumivu ya maungio ya mifupa
 • Kupooza
 • Kushindwa kufanya mambo (coordination problems)
 • Kushindwa kuhisi
 • Upofu
 • Kupoteza akili
 • Uhanithi
 • Kuharibiwa kwa neva za fahamu
 • Kuharibiwa kwa ubongo

Kuharibiwa kwa neva za fahamu (neurosphilis): ni hali inayoweza kutokea katika hatua yoyote ya ugonjwa kama neva za fahamu zikishambuliwa. Dalili zake ni pamoja na;

 • Maumivu makali ya kichwa
 • Kubadilika kwa tabia
 • Kushindwa kuhisi vizuri
 • Kushindwa kutawala kujongea kwa misuli
 • Kupooza
 • Ganzi
 • Kupoteza kumbukumbu

Vihatarishi vya kupata kaswende

Vitu vinavyoweza kukuongezea uwezekano wa kupata ugonjwa wa kaswende vinafanana sana na vile vya magonjwa mengine ya zinaa. Na hivi ni;

 • Kujihusisha sana na ngono isiyosalama
 • Ushoga
 • Kuwa na maambukizi ya Virusi Vya UKIMWI
 • Kuwa na mwezi mwenye ugonjwa wa kaswende
 • Kuwa na umri kati ya miaka 15-25

Ni muhimu kufahamu kuwa kama ukiwa na ugonjwa wa kaswende na ukatibiwa kikamilifu bado unaweza kupata maambukizi mapya. Hivyo hata baada ya matibabu chukua tahadhari usiambukizwe tena.

Vipimo

Vipimo vya kaswende katika hatua ya awali huhusisha uchunguzi wa vidonda na kupima maabara majimaji yanayotoka na kupima damu kuiabanini vaishiria vya kinga ya mwili. Kaswende inaweza kubainika siku 14 baada ya kupata maambukizi. Lakini kwa usahihi zaidi inaweza kuthibitishwa siku 90 baada ya kupata maambukizi. Majibu ya uongo kuwa mtu ana kaswende yanaweza kuonekana katika hizo siku 90 hasa kwa watu ambao wamewahi kuwa na kaswende katika siku za nyuma.[10]

Vipimo vya kaswende katika hatua ya 2-4 inahusisha kupima uti wa mgongo, moyo na damu kulingana na dalili zinazojitokeza kwa wakati huo.

Kama upatikana umeathirika, anza matibabu haraka na usifanyye ngono mpaka daktari akuruhusu kuwa sasa uko salama. Hakikisha unawaambia wenzi wako wa ngono wakapime na kupata matibabu.

Matibabu

ONYO: Maelekezo haya ya matibabu ni kwa ajili ya kutoa elimu na kujenga uelewa. Unahitaji usimamizi na maelekezo ya mtaalamu, usifanye mwenyewe!

Dawa ya kaswende mara nyingi ni penicillin. CDC wanapendekeza kwamba mgonjwa apate sindano za misuli za benzathine penicillin. Ni muhimu kufahamu kuwa matibabu haya yatasaidia kuua bakteria na kuzuia uharibifu zaidi lakini hayawezi kutibu uharibifu wa viungo uliokwisha fanyika.[11]

Kama unamzio na penicillin, unaweza kupewa doxycycline au azithromycin kama mbadala. Muda wa matibabu unatofautiana kulingana na kiasi ambacho mtu ameathirika, hatua ya ugonjwa na hali ya kiafya kwa ujumla.

Kama wewe ni mjamzito, penicillin ndio pekee salama kwako. Na endapo una mzio na penicillin utamwona mtaalamu akusaidie kuifanya penicillin isikudhuru ili uanze matibabu haraka. Dawa zingine zinaweza kumdhuuru mtoto na hazitazuia yeye kupata maambukizi.

maudhi yanayoambatana na matibabu

Ni kawaida kupata udhia wakati wa matibabu ya kaswende. Na dalili hizi zinatokana na kinga ya mwili kupambana na ugonjwa. Mara nyingi zinakuwa sio hatari sana, lakini kama ukiona zinakuletea shida zaidi fanya haraka kutafuta msaada wa kitabibu. Ndani ya siku moja ya kwanza ya mataibabu dalili zinazoweza kutokea ni pamoja na;[12]

 • Kutetemeka
 • Homa
 • Kujisikia vibaya
 • Kichwa kuuma
 • Maumivu ya maungio ya mifupa
 • Maumivu ya misuli
 • Kichefuchefu
 • Vipele

Wakati unaendelea na matibabu hakikisha unaepuka ngono mpaka malengelenge na vidonda vipone kabisa. Kama una mwezi wako hakikisha naye anapata matibabu. Usishiriki naye ngono mpaka amalize tiba.

Baada ya kumaliza matibabu ya kaswende, ni muhimu kupima damu mwezi wa 3, 5,12 na 24 kuhakikisha kuwa ugonjwa umeisha. Wapenzi lazima watibiwe wote; kaswende inaambukiza sana katika hatua ya kwanza nay a pili.

Tiba ya asili ya dalili za kaswende

Kaswende ni ugonjwa hatari. Ni lazima utibiwe na antibiotiksi kuhakikisha kuwa ugonjwa umeisha. Tiba ya asili ni nzuri kuondoa dalili za kaswende na dalili zinazoletwa na matibabu.

 1. Probiotksi

Unapokuwa ukitumia dawa, kula vyakula vyenye probiotiksi kwa wingi. Dawa huua bakteria wazuri na baketria wabaya. Ili kuwarudisha wale bakteria wazuri wanaoleta afya ni muhimu sana kutumia vyakula hivi. Mfano wa vyakula hivyo ni mtindi. kiwango kizuri cha probiotiksi utayochagua iwe bilioni 50 CFU. Pia vyakula vyenye probiotiksi vitawasaidia wanawake kutopata maambukizi ya fangasi ukeni.

 1. Vitamin B12

Unapokuwa unatibu magonjwa hatari kama kaswende, ni muhimu kula mlo kamili na kutibu upungufu wa vitamin au madini mwilini. Mara kwa mara imekuwa ikiwatokea watu wasiotumia nyama na mazao yake. Upungufu wa vitamin muhimu  kama hii husababisha dalili kuwa mzubaifu, kukosa nguvu, misuli kukaza, kuvurugika kihisia.

Vyanzo vizuri vya vitamin B12 ni samaki (hasa aina ya salmon na tuna), nyama ya ng’ombe, kuku, maini, mtindi na nyama ya kondoo mdogo.

 1. Mazoezi

Kujishughulisha wakati unaendelea na tiba ya kaswende itakusaidia kuondoa msongo, woga na sonona, itakusaidia kunyoosha misuli na kukupa nguvu. Kwa kuwa uchovu ni dalili innayotokea kwa wengi tafuta zoezi litakalokufaa.

 1. Kolajeni

Kaswende huathir afya ya akili na mwili, ngozi na maungio ya mifuoa na baadaye huathiri viungo vingine katika mwili. Matumizi ya vyakula vye kolajeni itasaidia kurejesha afya ya ngozi, mifupa, mwili na akili. Vyanzo vizuri vya kolajeni ni supu ya mifupa ya ng’ombe, nyama ya ng’ombe, mayai, kuku na samaki.

 1. Tangawizi

Tangawizi itakusaidia kuondoa kichefuchefu na kujisikia vibaya tumboni. Tengeneza chai ya tangawizi kisha ongeza asali na kunywa kila unaposikia kichefuchefu.[13]

 1. Masaji

Ni njia nzuri sana ya kuondoa maumivu, fadhaa na uchovu na pia kuimarisha kinga ya mwili wakati ukiendelea na matibabu ya kaswende. Masaji ya kitaalamu ya mara kwa mara itakusaidia kuuweka sawa mfumo wa limfu na ubongo, bila kuacha misuli na maungio ya mifupa. Fanya angalu kila mwezi mara moja na itapendeza zaidi kama ukifanya mara 2 kwa mwezi.[14][15][16]

 1. Krimu ya aloe na mrujuani kwa ajili ya vipele

Dalili nyingine inayosumbua sana wakati wa matibabu ya kaswende ni vipele. Ili kuondoa hivyo vipele tumia krimu hii itakusaidia.

Viambata:

 • ¼ kikombe cha jibini ya kokoa (cocoa butter)
 • 1/8 kikombe cha mafuta ya mbegu za zabibu (usiyatumie kwa kula)
 • 2 vijiko vya chakula vya udongo wa bentonite
 • 2 vijiko vya chakula vya aloe vera gel
 • 10 matone ya mafuta ya mrujuani (lavender essential oil)
 • 1-2 vijiko vya chakula vya witch hazel

Maelekezo

 1. Chemsha jibini ya kokoa kwenye kikaangio, changanya na mafuta ya mbegu za zabibu kisha iache iyeyuke huku ukichanganya taratibu.
 2. Ongeza aloe vera gel na koroga taratibu
 3. Toa motoni na oongeza udongo wa bentonite, witch hazel na mrujuani. Changanya taratibu
 4. Weka kwenye glass na ufunike vizuri
 5. Paka kwenye ngozi mara 2 kkwa siku, iache ikauke kwa dakika 15
 6. Osha taratibu kwa maji ya moto na kitambaa

Matatizo ynayoambatana na kaswende

Wajawazito na vichanga

Mama aliyeathirika na kaswende yupo katika hatari ya kuporomosha mimba, kuzaa mtoto aliyekufa au kuzaa njiti. Kuna hatari pia anaweza kumwambukiza mtoto wake kaswende. Kaswende ya kuzaliwa nayo kwa mtoto inaweza kugharimu uhai wa mtoto. Watoto wenye kaswende ya kuzaliwa wanakuwa na dalili hizi;

 • Ulemavu
 • Kudumaa katika kukua
 • Degedege
 • Vipele
 • Homa
 • Kuvimba kwa ini na wengu
 • Upungufu wa damu
 • Homa ya manjano
 • Malengelenge

Kama mtoto hataonesha dalili za kaswende mwanzoni, zitakuja kuonekana katika hatua ya mwisho ambapo mifupa, meno, macho, masikio na ubongo vitakuwa vimeharibika.

VVU

Watu wenye kaswende wanauwezekano mkubwa zaidi wa kupata Virusi Vya UKIMWI. Malengelenge ya ugonjwa yanaweza kurahisisha virusi kuingia mwilini.

Ni muhimu kufahamu pia wale wenye maambukizi ya VVU huwa na dalili za kaswende tofauti na wale wasio na maambukizi. Kama una VVU wasiliana na mtaalamu wa afya akusaidie kuzibaini dalili za kaswende.

Ni lini ukapime kaswende?

Mara nyingi dalili za awali za kaswende hua zinapotea bila mtu mwenyewe kujali au kujua. Dalili za hatua ya pili pia zinafanana na dalili za magonjwa mengine. Lakini ni muhimu kwenda kupima kama;

 • Ulifanya ngono bila kondomu na yeyote anayesadikika kuwa na kaswende
 • Ni mjamzito
 • Upo jera
 • Una mwezi aliyefanya ngono bila kondom na watu wengine.
 • Ni shoga

Neno la matumaini

Tunawezaje kutatua matatizo tuliyonayo? Ni Kristo pekee anayeweza kutusaidia. Anaweza akakufanyia vitu ambavyo usingeweza kujifanyia mwenyewe.

Leave a Comment

Your email address will not be published.